Total Pageviews

Search This Blog

Q Chief Achafukwa, Amporomoshea Matusi Diamond

Share it: MSANII nguli wa muziki wa kizazi kipya, Abubakar Katwila, maarufu kama Q Chief, ameamua kuvunja ukimya na kuulaumu uongozi wa Wasafi Media akidai kuwa wametumia picha na jina lake kwenye poster ya shoo yao ya Tumewasha na Tigo, Dar es Salaam bila kuwa na mawasiliano wala makubaliano naye.

 

Q Chilla amesema kuwa kitendo hicho kimemsababishia usumbufu huku akipigiwa simu na watu wakimuuliza kwa nini hakufika kwenye shoo hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia jana Januari 31, 2021, katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam.

 


Kupitia account yake ya Instagram, Chilla ameandika….. Habari Watanzania na industry yote ya muziki kwa ujumla. I think I need to address this issue to @diamondplatnumz @hellenkazimoto @sallam_sk na uongozi mzima wa @wcb_wasafi @tigo_tanzania.

 

 

Nimepokea simu nyingi sana jana mpaka today kuwa mbona sikuonekana kwenye show, as you all know muziki mimi ndo unanilisha na kuendesha mimi na familia yangu na pia niko na watu nyuma yangu (management) ambao wameniona mtu wa Ajabu sana.

 

 

“Kwani jina langu limeonekana kwenye poster ya #tumewashanatigo na nilikuwa kama one of the performer siku ya tarehe 30, Jan #uwanjawauhuru kitu ambacho sio kweli kwani sio mimi wala management ilizungumza na uongozi wa #wasafi kuhusu show hiyo.

 

 

“Nimejaribu kuwapigia lakini wanaleta sababu kwamba watu wamechoka kwasababu ya show. Hivo basi management yangu na mimi tumetoa siku ya leo kuwa ya mwisho kupata maelezo juu ya utapeli huu kutumia jina langu kupata fans wangu na wao kujiongezea credibility.

 

 

“Naomba @hellenkazimoto @diamondplatnumz mu act haraka on this kwani tutakuja laumiana. Sitaki matatizo na mtu napambana on my own naomba muwaeleze Watanzania either video or maandishi. Halafu hatua nyingine zitafata. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Asubuhi njema!

 

Aidha, kupitia video aliyoiposti, Chilla ameonyesha kuchukizwa na kitendo hicho huku akimporomoshea matusi mazito Diamond, Sallam Sk na Hellen Kazimoto (matusi makali ambayo hayawezi kuandikwa) na kutoa dakika tano kwa uongozi wa WCB kumuomba radhi na kuwaeleza wananchi kilichotokea.


Share it:

HABARI

Post A Comment:

0 comments: