Total Pageviews

Search This Blog

JPM Amrejeshea Hati ya Kiwanja Bibi wa Miaka 90

Share it:

 


Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli, ameagiza Bi. Elizabeth Sarali mwenye miaka 90, mkazi wa Manyoni mkoani Singida kurudishiwa umiliki wa eneo lake ambalo alipokonywa na kumilikishwa mfanyakazi wa idara ya ardhi.

 

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo akiwa njiani kurejea Dodoma leo Januari 31, 2021, aliposimama Manyoni mkoani Singida na kusikiliza kero mbalimbali, ikiwemo ya mgogoro wa ardhi baina ya mkazi mmoja na Halmashauri.

 

”Hili eneo ambalo nimeambiwa amepokonywa bibi Elizabeth Sarali mwenye miaka 90 kisha akamilikishwa mfanyakazi wa idara ya ardhi ambaye amepangisha Mnara wa Vodacom, hiyo hati ifutwe na arudishiwe umiliki huyo bibi aanze kulipwa pesa yake  ya pango na hao waliopanga” Rais Magufuli.

Aidha amewaagiza Mkuu wa mkoa, Wilaya na Ofisa Ardhi pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manyoni, kutatua mgogoro huo na mingine ya ardhi mara moja.

 

 

”Inaonekana Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manyoni hauna ‘information’, utadanganywa na watendaji kuhusu mambo mengi ya ardhi, shirikiana na Madiwani kutatua migogoro hii ya ardhi, sipendi madiwani ambao ni ‘Yes man’ kwenye kila kitu huwa sio wazuri”, amesema Rais Magufuli

Share it:

HABARI

Post A Comment:

0 comments: