Total Pageviews

Popular Posts

Search This Blog

Babu Tale, TRC Wazindua Barabara Ngerengere

Share it:

 

MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Kusini-Mashariki, Hamis Shabani Taletale, leo Desemba 5, 2020, amezindua ukarabati wa barabara ya kilometa 70.45 kutoka Ngerengere mpaka Mkurazi kwa usaidizi wa shirika la Reli Tanzania (TRC) ikiwa imepita takribani miaka 15 barabara hiyo kutofanyiwa ukarabati.

 

Taletale amesema, wakulima na wafanyabiashara watanufaika kwa barabara hiyo kukamilika maana itawarahisishia  shuguli zao za  kila siku na kusababosja kushuka bei za bidhaa mbalimbali.

“Tulianza na maji na sasa ni barabara, Nia yangu ni kuibadilisha Morogoro Kusini-Mashariki chini juu na juu chini, ili wananchi wafaidike na uongozi huu wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na jemadari Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema.

 

Aidha, Mkurugenzi mkuu TRC, Bi Jamila Mbarouk, amesema lengo la TRC ni kurejesha kile ambacho wanakipata kwa jamii katika utoaji wa huduma zao za kila siku, lakini ni fursa ya  kuwakumbusha wananchi kuwa reli hizi ni mali ya Watanzania, kila mwananchi ana haki na wajibu wa kuwa mlinzi wa miundombinu ya reli, akiwa na wajibu wa kuitunza, kuijali na kuithamini.


Share it:

HABARI

Post A Comment:

0 comments: