Total Pageviews

Search This Blog

Askofu Gwajima Kuzindulia Kampeni Bunju A, Jumapili

Share it:

 

Askofu Gwajima.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia CCM, Askofu Josepaht Gwajima anatarajia kuzindua kampeni zake keshokutwa Jumapili kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Bungu A, Jijini Dar.

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari leo mratibu wa kampeni za Mbunge huyo mtarajiwa, Paul Mfinanga alisema kampeni hizo zitazinduliwa kwenye viwanja hivyo na kuwataka wakazi wa jimbo hilo kuwasili kuanzia saa nne asubuhi.

Mratibu wa Kampeni za Askofu Gwajima, Paul Mfinanga wakati akitoa taarifa za uzinduzi huo kwa wanahabari leo (hawapo pichani).

Paul amesema sambamba na Askofu Gwajima mkutano huo utahudhuriwa na madiwani wa kata zote kumi za jimbo hilo ambapo nao wataeleza sera na mikakati yao ya kuleta maendeleo kwenye jimbo hilo.

Naye mwanaharakati na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Basihaya, Andrew Samson Gesugura amewataka wakazi wa mtaa huo na wananchi wa jimbo hilo kwa ujumla wahudhurie uzinduzi huo unaotarajiwa kuwa wa aina yake.

Mwanaharakati wa CCM ambaye pia Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Basihaya, Samson Gesugura (kushoto) naye akiwasisitiza wakazi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi.

Samson amesema wakazi wa ukombozi wa jimbo hilo umefika na kuwataka wakazi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo utakaokuwa salama na ulinzi wa kutosha kwa watu na mali zao.

Mkutano ukiendelea wasemaji hao wakiwa na wadau wa chama hicho.

“Uraisi tumpe Dkt. John Pombe Magufuli, Ubunge tumpe Askofu Gwajima na udiwani tuwape madiwani wetu ili kuunganisha nguvu moja kiutendaji na maendeleo ya haraka tuliyoyamiss na kuishia kuyaona kwenye majimbo ya wenzetu”. Alimaliza kusema Samson.

Pozi la ushindi.

Share it:

HABARI

Post A Comment:

0 comments: