Total Pageviews

Popular Posts

Search This Blog

Aliemtukana Rais Magufuli Facebook ahukumiwa

Share it:


Fadhili Silwimba, mkazi wa kijiji cha Nzoka Wilayani Momba Mkoani Songwe, amehukumiwa kulipa faini ya shillingi Millioni 5 au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kukutwa na hatia ya kumtusi Rais Wa Jamhuri ya Tanzania Dkt John Magufuli katika mtandao wa Facebook.

Hakimu Mkazi Mfawidhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe, Kassim Mkwawa amesema mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 23(I)na (II) cha mwenendo wa makosa ya kimtandao namba 4 ya mwaka 2015.

Awali mwendesha mashtaka wa Serikali Flavian Leonard Chacha, alisema kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo, mnamo Septemba 7, 2019, kwa kutuma ujumbe wa kumtusi Rais kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook.

Share it:

HABARI

Post A Comment:

0 comments: